Bunge la kaunti ya Narok limepitisha bajeti ya shilingi billioni 15.4. Kulingana na mwenyekiti wa bajeti Timothy Ole Maku na ambaye pia ni mwakilishi wadi wa Naikara ni kwamba kila sekta itapokea mgao kutoka kwa bajeti hiyo.

Kwa upande wake kiongozi wa walio wengi bungeni Songoi Lemein amewashukuru wawakilishi wadi kwa kupitisha bajeti hiyo na kutoa hakikisho kuwa watashirikiana ili kufanya maendeleo katika kaunti hii.

December 6, 2022