BY ISAYA BURUGU 6TH DEC 2022-Maafisa wa upelelezi wa jinai DCI huko Moro, Kunti ya Nakuru wameanzisha msako mkali  kumtafuta mwanamume aliyemuua  mpenziwe.Mshukiwa  Moses Njeri anaripotiwa kumdunga mpenzi wake Hannah Ndirangu mwenye umri wa miaka 28  kwa kisu kifuani kabla ya kutoroka kufuatia mgogoro ambao chanzo chake hakijabainika.

Majirani waligundua mwili wake wa mwanadada huyo baada ya kupata mpenyo kwenye nyumba hiyo ya mbao alilotumia mshukiwa huyo kutorokoea. Maafisa wa upelelezi wa DCI, walifika kwa kasi na kupata kisu cha kukatia mboga kilichokuwa na damu na kilichotumika kama zana ya mauaji.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika  hospitali ya kaunti ya Molo.

Haya yanajiri baada ya tukio lingine la kuhuzunisha kutokea eneo la Ongata Rongai kaunti ya Kajiado ambapo mwanadada mmoja alishikwa kwa madai ya kumuua mpenzi wake.

 

 

 

December 6, 2022