Bunge la seneti hii leo limeandaa kikao maalum ambapo wanajadili mustakabali wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Bunge hilo linatarajiwa kuidhinisha mswada ulopitishwa na bunge la kitaifa kuhusu jopo la uteuzi litakaloendesha zoezi la kuwateua makamishna wapya wa IEBC.

Mswada huo unapendekeza nafasi ya wawakilishi wa kidini kupunguzwa hadi moja ili nafasi iliyosalia ikabidhiwe kamati ya vyama vya kisiasa.

Na tukisalia katika bunge hilo ni kwamba William Kisang ameapishwa rasmi kama seneta wa Elgeyo Marakwet baada ya kushinda uchaguzi mdogo ulioandaliwa tarehe 5 mwezi huu.

Akitoa hotuba yake ya kwanza kama seneta, Kisang ameahidi kufanya Zaidi kuliko alivyofanya mtangulizi wake Kipchumba Murkomen ambaye sasa ni waziri wa barabara.

Kisang aliibuka mshindi baada ya kujizolea kura 41,378 kwenye kinyanga’anyiro kilichowavutia wagombea sita.

January 19, 2023