Chama cha Jubilee sasa kinajitambulisha kuwa chama huru, kisichohusishwa na muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja au Kenya Kwanza.

Haya yalibainishwa na kaimu kinara wa chama hicho Sabina Chege katika ukumbi wa Bomas of Kenya ambapo walikuwa wakiwasilisha mapendekezo yao mbele ya kamati ya kitaifa inayoongoza mazungumzo yanayoendelea ya pande mbili.

Chege alisema kuwa tayari wamempa spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula stakabadhi zinazohusu msimamo wao wa kisiasa ambao unabainisha kuwa hawana makubaliano rasmi na muungano wowote wa kisiasa.

Katika mapendekezo,Chege ameeleza kuwa masuala ya chama chochote cha kisiasa yasiingiliwe hasa baada ya Uchaguzi Mkuu.

Share the love
September 27, 2023