Mshukiwa wa Mauaji ya Eric Maigo Akamatwa.

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya Mkurugenzi wa Fedha katika Hospitali ya Nairobi Eric Maigo, amekamatwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka DCI, mshukiwa huyo, ambaye ni msichana mwenye umri wa miaka 16, alikamatwa usiku wa jana katika eneo la Kibera jijini Nairobi. Zoezi la kukamatwa kwake lilifanikishwa baada ya DCI kupokea taarifa kutoka kwa umma. Baada ya kukamatwa, mshukiwa huyo alisafirishwa hadi kituo cha polisi cha Muthaiga kwa uchunguzi zaidi.

Tukio la mauaji ya Bw. Maigo lilijiri tarehe 15 mwezi huu, ambapo alipatikana ameuwawa kwa kudungwa kisu nyumbani kwake. Kamera za CCTV zilizochapishwa na DCI zinaonyesha mshukiwa huyo akiruka ua la boma la marehemu Mkurugenzi Maigo.

 

Share the love
September 27, 2023