Chama cha mawakili LSK sasa kimemtaka mkurugenzi wa mashataka ya umma Noordin Haji kutoa sababu za kutupilia mbali kesi za ufisadi zilizokuwa zikiwakabili viongozi wa kisiasa ambao wameteuliwa kwa nyadhifa za mawaziri.

Haya yanajiri siku moja baada ya afisi ya mkurugenzi wa mashataka ya umma Kutupilia mbali kesi ya waziri mteule wa jinsia Aisha Jumwa.

Akizungumza na waandishi wa habari,mwenyekiti wa chama hicho Erick Theuri vilevile ameitaka idara ya mahakama kuingilia kati na kumshinikiza Haji kutoa sababu mwafaka kuhusiana na hatua ya kutupilia mbali kesi hizo.

SAUTI: MWENYEKITI WA LSK ERICK THEURI

October 13, 2022