Mahakama kuu ya Narok imetoa uamuzi kuwa hakuna mtu atakayerejea katika msitu wa mau .katika uamuzi ulitolewa na majaji watatu wa mahakama ya Narok akiwemo jaji Muhammad Kulow ,Jaji John Mutungi na jaji George Ong,ondo wamesema kwa kauli moja kesi iliyofikishwa mahakamani na wakili Kimutai Bosek kutaka watu waliofuruswa kutoka msitu wa mau kurejea katika msitu huo si halali.kulingana na majaji hao ni kwamba msitu wa mau ni chemichemi ya maji na kuna haja kuhifadhi mazingira kwa vizazi vijavyo.

SAUTI: KAULI YA MAJAJI

Kauli ya majaji hao imeungwa mkono na wakili Martin Kamwaro na Alan Meigati waliowakilisha marafiki wa mau wakisema mahakama hiyo imefanya haki kuamurisha watu wote kuondolewa katika msitu wa mau .Kamwaro amesema uamuzi huo ni wa haki kwa wenyeji wa kaunti ya Narok.

SAUTI: WAKILI KAMWARO

Aidha kuna baadhi mawakili ambao wamepinga uamuzi huo na kudai kuwa watakata rufaa.

October 13, 2022