Makamishena watatu wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini IEBC wanao ondoka ofisini wamesema kuwa hawana majuto yoyote kuhusu jinsi walitekeleza zoezi la uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka jana.

Makamishena hao ambao ni mwenyekiti Wafula Chebukati, Boya Molu na Abdi Guliye wamesema haya katika hafla ya kutoa ripoti yao kuhusiana na zoezi la uchaguzi, huku wakitarajiwa kuondoka ofisini baada ya muda wao wa kuhudumu kukamilika.

Chebukati alieleza kuwa nafsi yake imeridhika na jinsi uchaguzi uliandaliwa, akieleza kuwa tume hiyo ilikua imezingirwa na vishawishi vingi hasa asasi za serikali zilizotaka kuhitilafiana na matokeo ya uchaguzi. Chebukati amesema kuwa tume yake imemwandikia rais ikitaka kufanywa uchunguzi kuhusu matukio yaliyoshuhudiwa kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais.

Ripoti hiyo imetolewa siku moja tu kabla ya mwenyekiti wa tume hiyo wafula chebukati na makamishna wenzake wawili Boya Molu na Abdi Guliye kuondoka ofisini hio kesho.


Hotuba ya Mwenyekiti wa IEBC

January 16, 2023