Ripoti ya kitaifa kuhusu afya inaonyesha kuwa kaunti ya Samburu inaongoza katika visa vya ujauzito miongoni mwa watoto kwa asilimia 50.

Ripoti hiyo iliyotolewa na mamlaka ya takwimu nchini kwa ushirikiano na wizara ya afya imebaini kuwa kaunti zilizoathirika Zaidi na mimba za mapema ni pamoja na Pokot magharibi, Marsabit na Narok ambazo zina asilimia 36, 29 na 28 mtawalia.

Kando na hayo ripoti hiyo inaonyesha kuwa dhulma dhidi ya wanawake bado ni changamoto kubwa katika kaunti za Bungoma, Homabay, Murang’a, Samburu na Migori.

Aidha kulingana na ripoti hiyo, visa vya ukeketaji vimepungua kutoka asilimia 38 mwaka wa 1989 hadi asilimia 15.

January 17, 2023