Tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC imetoa ripoti yake ya mwisho kuhusu uchaguzi wa agosti 9 wa mwaka jana.

Ripoti hiyo imetolewa siku moja tu kabla ya mwenyekiti wa tume hiyo wafula chebukati na makamishna wengine wawili kuondoka ofisini.

Wadau wa sekta mbalimbali wamekuwa wakitoa tathmini yao kuhusiana na uchaguzi huo uliompa fursa William Ruto kuwa rais wa tano wa jamhuri ya Kenya.

Akizungumza wakati wa hafla ya kutolewa kwa ripoti hiyo, Chebukati amesema kuwa ingawa anamaliza atamu yake afisini, ameridhika sana na jinsi walivyoandaa uchaguzi huo na kuongeza  walistahimili dhoruba zilizotishia utendakazi wa tume hiyo. Kwa mara nyingine alieleza kuwa matokeo ya uchaguzi huo yaliakisi matakwa ya wakenya.

January 16, 2023