Naibu Rais Rigathi Gachagua ameeleza kwamba maafisa wa utawala uliopita wa Rais Uhuru Kenyatta waliiba Ksh.16 bilioni katika kipindi kilichopelekea kukabidhiwa kwa serikali ya Rais William Ruto.

Akizungumza jijini Nairobi Gachagua alisema pesa hizo zilikuwa zikisafirishwa kwa katoni kwa nyumba za watu fulani.

Gachagua alidokeza kuwa Ksh.10 bilioni ziliibwa wakati ambapo kesi ya uchaguzi ilikuwa ikiendelea huku Ksh.6 bilioni zikiibwa siku mbili tu kabla ya uchaguzi wa Agosti 9.

Gachagua aliendelea kulaumu madai ya wizi wa pesa za umma kwa sababu ya hali mbaya ya sasa ya uchumi.Alikariri kuwa serikali ya Kenya Kwanza ilirithi uchumi uliodorora kutoka kwa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.

March 4, 2023