Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC hii leo imefika mbele ya kamati ya mazungumzo ya maridhiano kati ya Kenya kwanza na Azimio ili kuwasilisha mapendekezo yao.

Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt. David Oginde alipendekeza tume hiyo kuongezewa wafanyakazi Zaidi ili kuiwezesha kukabiliana na kesi za ufisadi haraka iwezekanavyo.

Wengine waliowasilisha mapendekezo yao ni Baraza la maaskofu wa kikatoliki nchini KCCB, ambao wamependekeza kutafutwa kwa namna ya haraka ya kusuluhisha matatizo yanayozingira sekta ya afya nchini.

KCCB imependekeza kuangaziwa upya kwa mfumo wa bima ya afya ya kitaifa ili kuwawezesha wakenya wengi zaidi kuweza kufaidika na mpango huo.

 

Share the love
October 3, 2023