Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC, imezindua mipango yao ya utendakazi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo katika ukumbi wa KICC.

Afisa mkuu mtendaji wa EACC Twalib Mbarak akizungumza katika hafla hiyo, amesema kwamba ufisadi ni adui mkubwa kwa kila mmoja katika taifa la Kenya, huku akitupilia mbali dhana kwamba ufisadi unaendelea kuenea kwa sababu wanaohusika hawaonekani.

Mbarak amesema kwamba mataifa yanayokua yanashuhudia kiwango cha juu cha ufisadi ikilinganishwa na mataifa yenye uchumi mkubwa. Wengine waliohudhuria uzinduzi huu ni pamoja na mkuu wa mawaziri nchini Musalia Mudavadi pamoja na viongozi wengine wa kisiasa na pia kutoka idara ya mahakama nchini.

Share the love
September 26, 2023