BY ISAYA BURUGU,26TH SEPT,2023-Jamii ya kaunti ya Narok imetakiwa kukumbatia taasisi za kiufundi hasa kwa wanafunzi waliokamilisha darasa la nane na kidato cha nne.

Wito huu umetolewa na mwenyekiti wa taasisi ya kiufundi ya Maasai Mara Gabriel Tanyasis.Akizungumza wakati wa ukaguzi wa  taasisi ya kiufundi eneo la Olereko Trasmara magharibi Tanyasis ametoa wito kwa wenyeji wa kaunti ya Narok kuwasaidia wanafunzi kujiunga na vyuo vya kiufundi ili waweze kupata  mafunzo ya kujimudu kimaisha.

Wakati huo huo mwenyekiti huyo amesema wanatarajia kufungua taasisi hiyo juma hili katika hatua ya kuhakikisha wanafunzi waliokamilisha masomo yao eneo la Trasmara magharibi wanapata elimu ya kiufundi

Katibu mkuu wa kudumu katika wizara ya elimu nchini Beliong Kapsang na katibu wa kudumu katika sekta utalii nchini John Oloontua wataongoza ufunguzi ya chuo hicho.

 

 

 

 

 

 

 

Share the love
September 26, 2023