BY ISAYA BURUGU 18TH AUG 2023– Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC sasa inasema kuwa uajibikaji kwa rasilimali za umma bado ni changamoto kubwa kwa serikali za kaunti.Wakizungumza katika mkutano wao kaunti ya Mombasa,

mwenyekiti wa tume hiyo David Oginde amesema kuwa kwa muda wa miaka kumi  ya ugatuzi wanachunguza kesi alfu 10 kutoka kaunti mbali mbali zinazohusiana na ubadhirifu wa fedha za kaunti na usimamizi mbaya wa rasilimali za kaunti ,nyingine ni ulaghai wa ununuzi,ulaghai wa mishara haswa kupitia kwa wafanyikazi hewa,ulaghaia wa ulipaji wa madeni na kupuuza sheria zinazohusiana na usimamizi makini wa mashirika ya umma.

Tayari mashirika ya kupambana na uhalifu yamehusishwa kuchukua hatua.

 

 

 

 

 

 

August 18, 2023