MP. John Kiarie

Wabunge katika bunge la kitaifa,wamependekeza sheria mpya ya upanzi wa miti kando mwa barabara baada ya kukatwa kwa miti wakati wa utengenezaji wa barabara katika maeneo yote ya taifa.

Wabunge walikua wakiujadili mswada wa mbunge wa Dagoretti Kusini John Kiarie ambaye alipendekeza kuwekwa kwa kigezo kitakachowalazimu watengezaji wa barabara kuwa na mipango ya upanzi wa miti baada ya kumaliza shughuli za ujenzi wa barabara.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha hoja yake bungeni, Mhe. Kiarie aliweka wazi kuwa wakenya wana haki ya kupata hewa safi, jambo ambalo linaathiriwa kwa ukosefu wa idadi ya juu ya miti kote nchini. Katika wasilisho lake, Mbunge huyo aliweka bayana kwamba mswada huo umekuja wakati mwafaka huku ulimwengu ukiendelea kujadili mikakati ya kuimarisha maswala ya tabianchi na kupunguza athari zake katika mkutano wa umoja wa mataifa wa COP27.

Mbunge huyo amependekeza wanakandarasi wote wanaohusika katika shughuli za ujenzi wa barabara, kulazimishwa kupanda miti ili kuirejesha miti iliyokatwa wakati wa ujenzi wa barabara, akiongeza kwamba mandhari ya maeneo mengi pia yameathiriwa baada ya ujenzi wa barabara.

Sikiliza Vipindi vyetu Moja kwa moja!

--:--
--:--
  • cover
    Osotua Live Stream
November 10, 2022