Raila Odinga

Kinara wa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga ameishutumu serikali kwa kuunga mkono uvunjaji wa sheria na pia kwa kile alichokitaja kama hulka ya kutojali.

Katika taarifa yake mapema leo, Bwana Odinga, pia ameisuta ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kwa kufuta kesi dhidi ya maafisa wa serikali pamoja na watu wengine wenye uhusiano wa karibu na viongozi wa serikali, akikashifu pia  kuongezeka kwa matukio ya uhalifu akisema kwamba haya yote yanaashiria kuwa taifa linaelekea katika siku za hapo nyuma bada la kupiga hatua mbele.

Kiongozi huyo aidha amesuta hulka ya kuandamwa kwa baadhi ya maafisa wa idara ya DCI, akiongeza kuwa ipao hali hii itanendelea, huenda hali ya usalama ya taifa ikadidimia hata Zaidi.

November 10, 2022