Mamlaka ya kudhibiti bei ya mafuta humu nchini EPRA imezindua msururu wa kampeni za kuwahamasisha wananchi kuhusu matumizi yanayofaa ya kawi ili kuepuka ajali za mara kwa mara.

Mamlaka hiyo imeanzisha kampeni hiyo ili kuwaonya wananchi dhidi ya kufyonza mafuta katika lori za kusafirisha mafuta au kukimbia kuteka mafuta haya katika Mikasa nayohusisha magari haya. Mkurugenzi Mkuu wa EPRA Daniel Kiptoo, amesema kuwa mikasa ya moto inayoshuhudiwa inatokana na hulka ya wakenya katika ununuzi wa mitungi ya Gesi pamoja na tabia ya kukimbia katika maeneo yaliyoshuhudia ajali zinazohusisha gari za kusafirisha mafuta.

EPRA ambayo itashirikiana na wizara ya kawi nchini pia inapania kutumia kampeni hizi kuwarai wananchi kutafuta huduma za wahandisi wa stima waliofuzu na kuidhinishwa.

November 18, 2022