Rais William Ruto hii leo amezindua mradi wa ujenzi wa barabara ya mtwapa-kilifi ambayo inatarajiwa kurahisisha usafiri baina ya kaunti za Mombasa na Kilifi. Rais Ruto amesema kuwa barabara hiyo ya kilomita 40 itapunguza kero la msongamano wa magari sawa na kuimarisha usalama wa watembea miguu kwani itajumuisha madaraja sita yatakayotumiwa kama kivukio kutoka pande moja hadi nyingine. Viongozi walioandamana na Ruto nao wamepongeza hatua hiyo na kudokeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo utainua uchumi wa kanda la pwani.

Wakati huo huo, Rais amesema Serikali itaziba mianya inayochochea matumizi ya dawa za kulevya nchini , hususan katika Mkoa wa Pwani.

November 19, 2022