Maafisa wa polisi katika eneo la Kasarani wamewatia nguvuni washukiwa sita wa ujambazi wanaohuishwa na visa vya uhalifu katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi.Washukiwa hao sita wa ujambazi wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kasarani.

Washukiwa hao walikamatwa  wakati wa msako wa usalama Santon ambapo walipatikana wakiwa na bunduki na simu tisa. Maafisa wa usalama wameimarisha doria jijini Nairobi na viungani mwake kufuatia kuongezeka kwa msururu wa visa vya uhalifu na uvamizi dhidi ya wakaazi.

Kwingineko maafisa wa polisi katika eneo la Tigoni kaunti ya Kimabu wamefanikiwa kupata simu za rununu elfu tatu zinazoaminika kutumika na matapeli kuwalaghai wakenya.Kando na hayo, maafisa hao wamepata rekodi zinazoonyesha matapeli hao waliwalaghai wakenya shilingi milioni 60.

November 18, 2022