CO27

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yanapania kukubaliana kuhusu msimamo wao wa pamoja, katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo suala linaloleta mvutano la fidia ya fedha kwa uharibifu unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi katika mataifa masikini duniani.

Mataifa ya Umoja huo, ambayo ni ya tatu kwa utoaji wa gesi chafu, yanaendelea kushinikizwa na mataifa yanayoendelea kulegeza msimamo wao na kukubali kutoa fidia kwa mataifa yanayopitia uharibifu mkubwa unaosababishwa na mafuriko, ongezeko la kina cha maji ya bahari na athari nyengine zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Taarifa zinadokeza kuwa msimamo wa Umoja wa Ulaya katika mkutano huo wa kilele wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi Novemba, inaonesha kuwa nchi 27 wanachama  wa Umoja wa Ulaya zitaunga mkono mazungumzo juu ya mada hiyo katika mkutano wa COP 27 nchini Misri.

October 24, 2022