LSK na rais Ruto

Chama cha Wanasheria nchini LSK Kimeeleza kuunga mkono msimamo wa Rais William Ruto dhidi ya mauaji kiholela na ukiukaji wa haki za binadamu, huku wakipendekeza kuundwa kwa tume ya uchunguzi itakayoshughulikia kesi za aina hii.

Wanasheria hao walitoa mapendekezo haya katika kikao na Rais Ruto kilichoandaliwa katika ikulu ya rais jijini Nairobi. Kwa upande wake Kiongozi wa taifa amesisitiza kuwa serikali yake itaheshimu sheria akisema kuwa kuwa demokrasia itaimarika tu iwapo kila mmoja atafuata sheria, huku pia akieleza kuwa uongozi wake hautahitilafiana kwa vyovote na taasisi huru.

Rais Ruto aidha amekubali pendekezo la LSK la kusaidia katika kuandaa na kusaini mikataba ya kibiashara na mataifa mengine.

October 24, 2022