Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Uteuzi imewasilisha ripoti ya zoezi la msasa wa mawaziri wateule 24 siku chache baada ya zoezi hilo kukamilika.Kamati hiyo imetupilia mbali uteuzi Penina Malonzo kama waziri mteule wa utalii huku mawaziri wateule waliosalia wakiidhinishwa na wabunge. Aidha viongozi wa wachache bungeni vilevile waliitaka kamati hiyo kutupilia mbali uteuzi Aisha Jumwa kama waziri mteule wa jinsia pamoja na uteuzi wa Mithika Linturi kama waziri mteule wa kilimo.

Majina ya mawaziri hao wateule yatawasilishwa kwa rais William Ruto kwa uteuzi rasmi kisha baadaye wataapishwa ili kutwaa naydhifa hizo za mawaziri.

October 25, 2022