BY ISAYA BURUGU,28TH OCT,2023-Gavana wa kaunti ya Kajiado Joseph Olelenku amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kushiriki upanzi wa nyasi na chakula cha mifugo wakati huu wa kipindi cha mvua ili kujiepusha na makali ya kiangazi  jinsi ilivyoshuhudiwa hivi maajuzi.

Gvana huyo amesema Kajiado ilipoteza Zaidi ya mifugo laki tano kutokana na uhaba wa chakula na maji na sasa ni wakati mwafaka kwa wakulima kuanza kuweka mikakati ya kupata malisho na maji ili waweze kuitoa kwa mifugo wao.

Pia amewataka wakaazi kuchangamkia upanzi wa miti haswa ya matunda ili kupiga jeki azimio la serikali kupanda mitio bilioni 15 ifikiapo mwaka 2030 na pia matunda hayo yatatumika kama lishe wakati wa kiangazi.

 

 

 

Share the love
October 28, 2023