Ruto-Comoros Congo

BY ISAYA BURUGU,28TH OCT 2023-Rais William Ruto aliondoka nchini jana jioni kuhudhuria kongamano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa nchini Kongo Brazzaville.

Mkutano huo wa siku tatu, unaojulikana kama Mkutano wa Mabonde Matatu umeandaliwa na Umoja wa Mataifa na kuwaleta pamoja viongozi kutoka mikoa ya Amazon, Kongo na Borneo-Mekong-Kusini Mashariki mwa Asia ili kuunda muungano wa kimataifa.

Kulingana na tovuti rasmi ya Mabonde Matatu, maeneo haya matatu pekee yanachukua asilimia 80 ya misitu ya kitropiki duniani na theluthi mbili ya viumbe hai wa nchi kavu, ikitekeleza  jukumu muhimu katika kudhibiti usawa wa kaboni.

Mkutano huo unalenga kutekeleza, ndani ya mfumo wa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Marejesho ya Mfumo wa Ikolojia, muungano wa kwanza wa kimataifa kurejesha hekta milioni 350 za mifumo ikolojia ya nchi kavu na majini.

Mkutano huo pia unawashirikisha Wakuu wa Nchi, Wajumbe Rasmi, Wawakilishi wa Serikali, Taasisi za Kimataifa, Wafadhili, Mashirika ya Fedha na wataalam

October 28, 2023