By Isaya Burugu,Oct 12,2022-Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu ametaja baraza Lake la mawaziri linalowajumuisha waliolambishwa sakafu kenye uchaguzi mkuu wa Agosti tisa baada ya kuwania  viti mbali mbali.

Baraza hilo linamujumuisha John Gatua aliyewania uwakilishi wadi wa Narok Mjini kwa tiketi ya chama cha Service Party na kupoteza kwa Lucas Kudate wa ODM .Pia kunao waliohudumu kwenye serikali ya kaunti iliyopita yake aliyekuwa gavana Samuel Tunai.

Walioteuliwa ni David Mutet ambaye ni  waziri wa fedha ,waziri wa afya ni Anthony  Namungukuk wazari utalii ni Jackson Sereni ,Kilimo ni Joyce Keshe ,waziri wa elimu ni Robert Simotwo, Waziri wa ardhi Sereti Mpeti ,waziri wa mawasiliano na tecknologia Linus Nairimo ,waziri wa uchukuzi John Gatua ,waziri wa leba Josphine  Chepgeno huku John Tuya akikabidhiwa nafasi ya katibu wa kaunti  ya  Narok , Rotic Kilangat ameridhika na wiziri ya mazingira.

Ntutu amesema sasa walioteuliwa watafika mbele ya bunge la kaunti ya Narok kupigwa msasa Wakati huo huo Ntutu amesema baraza hilo ni uso ya kaunti ya Narok na kila jamii imewakilishwa katika baraza hilo.

Ntutu amesema serikali yake inapania kuleta mabadiliko katika sekta mbali mbali kaunti ya Narok. 

 

 

October 12, 2022