BY ISAYA BURUGU,1ST MARCH,2023-Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ole Ntuntu amezindua mpango wa maendeleo ukiwemo usambazaji wa maji wenye dhamani ya shilingi  bilioni moja nukta tatu kwenye awamu ya kwanza.

Akizungumza katika eneo kuu la Kichinjio cha Olpopongi,gavana huyo amesema kuwa jumla ya shilingi bilioni tatu zimetengwa kwa minajili ya usambazaji maji katika wadi zote thelathini za kaunti ya Narok.Gavana Ntutu amewahakikishia wakaazi wa Narok kuwa muradi huo wa maji utaongeza kiwango cha usambazaji maji na kwamba tatizo hilo litakabaliwa kiamilifu hivi karibuni.

 

March 1, 2023