BY ISAYA BURUGU,1ST MARCH,2023-Kenya imeungana na ulimwengu hivi leo kuadhimisha siku ya viti vya magurudumu duniani kwa walemavu.Humu nchini maadhimisho hayo yameandaliwa katika kituo cha walemavu cha  bombolulu kaunti ya Mombasa.

Maadhimisho hayo yanalenga kutoa hamazisho,ya umuhimu wa kiti cha magurudumu kwa walemavu na kuhakikisha kuwa kila mlemavu anapata kiti hicho licha ya hali yake ya kimaisha.Maadhimisho hayo yameanza kwa matembezi kutoka barabara kuu ya Mombasa kuelekea Malindi ili kutoa hamazisho kwa wakaazi sawa na ulimwengu kwa ujumla.

Kwa mjibu wa Benson Agesa kutoka shirika linalowashughulikia walemavu nchini LPDK ni kwamba kenya inahitaji viti laki moja kila mwaka vya maguruduu hitaji ambalo sio rahisi kuliafikia kwnai gharama ya viti hivyo ni yajuu mno.

Inagharimu shilingi alfu 25 kununua kiti hicho.

.

 

 

 

 

 

 

March 1, 2023