Mwanasiasa wa Kiambu Gladys Chania na mshukiwa mwenza Maurice Mbugua wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja pesa taslimu kila mmoja. Chania na Mbugua wanashtakiwa kwa kupanga mauaji ya kikatili ya mumewe, mfanyabiashara George Mwangi. Idara ya Upelelezi wa Jinai ilikuwa imewasilisha ombi la kuwazuilia wawili hao kwa siku saba Zaidi ila hakimu mkuu Wilson Rading’ alikataa ombi hilo. Washukiwa hao wawili walikuwa wamezuiliwa kwa siku saba ili kuruhusu DCI kukamilisha uchunguzi.Maafisa wa upelelezi walimkamata Chania mnamo Oktoba 14. Wapelelezi walisema Chania anaaminika kupanga mauaji ya mumewe baada ya kujua kuhusu madai ya mapenzi ya mumewe na katibu wa shule moja kiambu. Mwangi, 58, alikuwa mwanakandarasi nchini Rwanda na aliwasili nchini Septemba 13.

 

 

October 24, 2022