Hatimaye rais William Ruto amevunja kimya chake kuhusu suala tete linalohusu uamuzi wa mahakama ya juu ambao uliwapa idhini wanachama wa LBTQ kujumuishwa kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa hazina ya kustawisha biashara za akina mama, rais Ruto amewataka wakenya kutokuwa na wasiwasi akiwahakikishia kwamba uamuzi huo hautatekelezwa humu nchini huku akiwataka viongozi wa dini kusimama kidete na kupigania maadili ya taifa hili.

Kauli yake Ruto imeungwa mkono na naibu wa rais Rigathi Gachagua ambaye ameeleza kuwa uamuzi huo unakiuka bibilia na tamaduni za kiafrika.

 

March 2, 2023