BY ISAYA BURUGU,9TH SEPT,2023-Idadi ya watu walioaga dunia katika ajali ya barabarani iliyohusisha matatu katika Barabara kuu ya Kajiado kuelekea Namanga imefikia watu wanne baada ya watu wawili kufakiri walipokuwa wakipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kajiado.

Wawili hao walikuwa miongoni mwa abiria 13 waliokuwa wamepata majeraha mabaya.

Miili ya wawili hao Pamoja na wengine wawili walioaga dunia katika eneo la tukio kwa sasa inahifadhiwa katika makafani ya hospitali ya rufaa ya Kajiado.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia leo ambapo gurudumu la gari la chama cha ushirika cha NAEKANA lilipasuka karibu na kiwanda cha KEDA baada ya kukosa mwelekeo na Kubingiria mara kadhaa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share the love
September 9, 2023