ODM

Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, ametetea amuzi wa chama chake cha ODM, wa kuwafurusha baadhi ya viongozi waliokuwa katika chama hicho.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kaunti ya Migori Siku ya Ijumaa, Odinga aliweka wazi kwamba viongozi ambao wamekuwa wakiruka kutoka chama kimoja kwenda kingine wanastahili kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Siku ya Jumatano wiki hii, chama cha ODM kilifanya uamuzi wa kuwafurusha viongozi watano inaosema kwamba walikuwa wakishirikiana na serikali.

https://twitter.com/RailaOdinga/status/1700171909315404017?s=20

Katika tangazo lingine, chama cha ODM kilitangaza mageuzi katika uongozi wa ofisi kuu ya kitaifa ya chama hicho. Mageuzi haya yanajiri saa chache tu baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Kitaifa cha chama siku ya Jumatano.  Katika mageuzi yaliyotangazwa, Gavana wa Kisii Simba Arati amekabidhiwa wadhifa wa naibu mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho, akitwaa wadifa uliokuwa ukishikiliwa na mwakilishi wa kike wa Kaunti ya Kisii Janet Ong’era.

Mabadiliko mengine ya uongozi yaliyotangazwa na ODM, Catherine Omanyo sasa ndiye naibu wa katibu mkuu wa chama hicho, wadgifa uliokuwa wa Florence Mutua. Mbunge wa Saboti Caleb Amisi ametwikwa jukumu la kuwa naibu wa Ktibu wa mipango chamai humo, huku Fatuma Masito akiteuliwa kuwa naibu wa kitaifa wa mweka hazina

 

September 8, 2023