BY ISAYA BURUGU,04,NOV 2022-Ripoti ya utenda kazi wa mahakama nchini sawa  na utekelezaji  wa haki iliyozinduliwa leo imebainisha kuwa upungufu wawafanyikazi wa idara hiyo ndio kikwzzo kikuu katika utekelezaji jukumu lake.Cecilia Kabura ana mengi Zaidi.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa katika majengo ya mahakama ya juu inaelezea hali halisi ya mambo katika idara ya mahakama katika kipindi cha mwaka mmoja uliyopita na yale yanayosalia kufanywa.Huyu hapa jaji kuu Martha Koome.Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa sheria Justin Muturi amesema kuwa  ni wazi kwamba kumekuwa na juhudi zilizowekwa kuhakikisha kuwa idara ya mahakama inafurahia uhuru wake kama inavyohitajika kikatiba.Muturi akiongeza kuwa  utekelezaji wa hazina ya idara ya mahakama  na mgao wa shilingi bilioni 3 uliyo ongezwa  kila mwaka pia ni muhimu.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Nairobi Johnstone Sakaja amesema kuwa juhudi zote zinapaswa kuelekezwa katika kufanikisha utoaji huduma za haki kwa haraka  na kuwataka wahusika kushirikiana katika kufanikisha ujenzi wa mahakama Zaidi.

Rais Wiliam Ruto,naibu wake Rigathi Gachagua ,mkuu wa sheria Justin Muturi na spika wa bunge la Kitaifa Moses Wetangula ni miongoni mwa waohudhuria.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

November 4, 2022