Inspekta jenerali wa polisi Japheth Koome amesema kuwa idara ya polisi iko ngangari kukabiliana na visa vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa katika miji mbalimbali. Kwenye kikao na waandishi wa habari, Koome amedokeza kuwa watatumia njia zote walizo nazo kushughulikia wizi kwa kutumia vurugu kwani ni hatia.

Koome vilevile ameongeza kuwa wahalifu watahudumiwa kama wahalifu na kuwarai wanasiasa kutoleta siasa kwa mambo ya polisi.  Aidha amewapa makataa ya wiki moja vijana ambao wana bunduki kinyume cha sheria kurejesha bunduki hizo.

Naye kwa upande wake gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameahidi kushirikiana na idara ya polisi ili kupunguza visa vya uhalifu katika kaunti hiyo.

November 14, 2022