BY BURUGU ISAYA,3RD JAN 2023- Inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome amekiri kubadilishwa kwa walinzi wa rais mustaafu Uhuru Kenyatta.Akizungumza na wandishi Habari hivi leo,

Koome hata hivyo amepuuzilia mbali madai kwamba ulinzi wa rais Mustaafu Uhuru Kenyatta ulikuwa umeondolewa.

IG amesema mabadiliko hayo hayana kinyongo na si ya kulipiza kisasa bali ni kuambatana na sheria za nchi.Alieleza kuwa kulingana na sheria afisa mkuu wa ulinzi wa rais Mustaafu anafaa kuwa wa cheo cha chini na sio naibu inspekta wa polisi ili pawepo utaribu mwafaka katika kutoa maagizo ya kazi.

Koome vile vile amekiri kuwa usalama wa Uhuru ulipunguzwa ili kuambatana na hadhi yake ya sasa kama rais mustaafu.Amewaeleza wakenya kuwa kamwe usalama wa Uhuru hauwezi kuondolewa kwani ni haki yake kama rais mustaafu kupewa ulinzi na serikali.

Amethibitisha kuwa bado familia na makazi ya waliokuwa maraisi bado zinapewa uinzi wa kutosha.

Mkuu huyo wa polisi pia alithibitisha mabadiliko makubwa katika ulinzi wa waliokuwa mawaziri chini ya serikali ya Uhuru Kenyatta. Alisema kuwa walipunguza ulinzi wa maafisa hao ili kuiana na majukumu yao.

February 3, 2023