BY ISAYA BURUGU,3RD FEB 2023-Fredrick ole Leliman, afisa wa polisi anayeaminika kupanga mauaji ya wakili  Willie Kimani, mteja wake  Josephat Mwenda na mwendesha texi  Joseph Muiruri mwaka 2016 amehukumiwa kifo.Waliokuwa wafanyikazi wenzake na watuhumiwa   Stephen Cheburet Morogo na Sylvia Wanjohi ambao pia walipatikana na hatia ya mauaji wamehukumiwa kifungo cha miaka  30 na  24 mtawalia.

Wakati huo huo aliyekuwa akiwapasha Habari  na kufanikisha mauaji hayo  ya watu watatu amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

Akitoa hukumu hiyo jaji  Jessie Lessit amesema mauaji ya wakili Willie Kimani, Mteja wake  Josephat Mwenda na dereva  Joseph Muiruri kilikuwa kitendo cha kinyama ambacho hakipaswi kushudiwa kamwe .Watuhumiwa wana siku 14 kukata rufaa.

Wakili Willie Kimani, mteja wake  Mwenda na mwendesha texi walitekwa nyara  walipokuwa wakitoka kataiaka mahakama ya Mavoko  kaunti ya Machakos  mnamo tarehe 23 mwezi Juni mwaka 2016  ambapo Mwenda alikuwa amewasilisha kesi dhidi ya afisa wa polisi.

February 3, 2023