Naibu wa rais Rigathi Gachagua, alikuwa mgeni katika kikao kilichowaleta pamoja magavana kutoka mkoa wa Bonde la Ufa, waliokuwa wakijadili na kuweka mikakati inayofaa kabla ya kuandaa siku ya kitaifa ya maombi tarehe 12 mwezi huu.

Katika taarifa yake baada ya kuhudhuria kikao hicho, Naibu wa rais alieleza kuwa dhima ya maombi haya itakuwa kutoa shukrani baada ya uchaguzi wao mwaka jana, na pia kwa amani inayoendelea kushuhudiwa humu nchini.

Aidha aliweka bayana kuwa kiongozi wa taifa rais William Ruto atahudhuria hafla yenyewe.

February 2, 2023