Jaji Mkuu Martha Koome amepongeza Mahakama ya Mizozo ya Vyama vya Kisiasa kwa kutatua kwa haraka mizozo ya kabla ya uchaguzi.

Koome ameeleza kuwa Mahakama hiyo ilihakikisha migogoro yote 314 ya kabla ya uchaguzi inatatuliwa kwa wakati.

Kulingana naye, mahakama hiyo inaendelea kuunga mkono malengo ya idara ya mahakama ya Mabadiliko ya Kijamii kupitia Haki kwa kuhakikisha wakenya wanapata haki kwa wakati unaofaa.

Aidha Koome ameongeza kuwa walijifunza mambo mengi muhimu ambayo yatawasaidia kutekeleza azma ya kusambaza faili za kielektroniki nchini kote kwa mahakama.

Share the love
January 10, 2023

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

%d bloggers like this: