BY ISAYA BURUGU   10TH JAN,2023-Serikali imetakiwa kufanya uchuguzi kuhusu visa vya ulaghai wa ardhi ya umma vinavyoriopotiwa kukidhiri mjini Narok.Ni wito wake aliyekuwa mwaniaji wa kiti cha ubunge Narok kaskazini  Kerempoti Sadera .

Sadera akizungumza mjini Narok amesema swala ardhi ni swala nyeti hivyo basi kuna haja ya serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha ardhi haswa ardhi ya umma inalindwa .Kwa mjibu wa Sadera, kuna baadhi ya wahusika ambao wamenyakua ardhi ya umma huku  baadhi ya watu kutika mji wa Narok wakidai kutapeliwa ardhi yao.

Sadera amesema wamekutana na idara mbali mbali za serikali ikiwemo idara ya upelelezi wa jinai DCI, idara ya ardhi na ofisi ya kaunti kamishana wa Narok ili kuthamni swala la ardhi katika eneo la Total viungani mwa mji wa Narok.

Hayo yanajiri baada ya  baadhi ya wenyeji mjini Narok kulalamikia unyakuzi wa ardhi Sadera amesema lazima haki ipatikane kwa maswala ya ardhi mjini Narok.

 

 

January 10, 2023