Jaji mkuu Martha Koome ameshikilia kwamba uhuru wa idara ya mahakama hautaingiliwa kwa namna yoyote. Kwenye kikao na waandishi wa habari baada ya kufanya mkutano na rais William Ruto huko Naivasha, Koome hata hivyo amesema kuwa idara hiyo iko tayari kufanya mazungumzo ya kujadili changamoto zinazokumba idara hiyo.

Hotuba ya koome inajiri baada ya kukamilika kwa mkutano wa wakuu wa idara ya mahakama.

 

February 21, 2024