Rais William Ruto amesema kuwa Kenya imepiga hatua kubwa katika kujiondoa kwenye orodha ya mataifa yasiyotilia mkazo ulipaji wa madeni yake.

Akiwahutubia waandishi wa habari katika eneo la Naivasha baada ya kukamilika kwa mkutano wa mawaziri, kiongozi wa taifa amesema kwamba taifa la Kenya limejinasua na kufanikiwa kujiondoa kwenye kitengo hicho na sasa ina uwezo wa kuaminika na wawekezaji kutoka sehemu zote za dunia.

Kuhusu suala la uagizaji wa chakula kutoka nje,  rais Ruto ameeleza kuwa serikali inapania kupunguza uagizaji huo kwa asilimia 50 katika kipindi cha miaka 5 ijayo, na kuhakikisha kwamba katika kipindi cha miaka 10 ijayo, Kenya haitakua ikiagiza chakula chochote kutoka nje.

February 21, 2024