BY ISAYA BURUGU,26TH SEPT,2023-Shughuli za kimatibabu katika hospitali za umma kaunti ya Nakuru zimetatizika leo baa da ya Madakitari katika kaunti ya  kuanza  mgomo wao kulalamikia kile wanachosema ni kukosa kutekelezwa kwa mkataba wao wa kuboresha mazingira ya utenda kazi wao na mwajiri wao.

Kati ya malalamishi ya madkitari hao ni Pamoja na kutopandishwa vyeo,mishahara duni na ukosefu wa vifaa vya kutosha vya utenda kazi.

Naibu katibu mkuu wa KMPDU Denies Misikela maesema kuwa madakitari hao wapatao 209 hawatarejea kazini hadi mktaba wao wa Pamoja wa mwaka 2017 utekelezwe.

Madakitari hao pia wanaitisha kuajiriwa kwa madakitari mia moja Zaidi ili kukabiliana na upungufu mkubwa wa madakitari unaoshuhudiwa katika hospitali za umma katika kaunti hiyo.

 

 

 

September 26, 2023