BY ISAYA BURUGU ,17TH NOV 2022-Wakaazi wa Ruaka  eneo la Kiambu, waligutushwa na kuporomoka kwa jengo la ghorofa 5 lilokuwa  likijengwa.Jengo hili ambalo limeanguka karibu na eneo ya  Fortune Club liliangukia nyumba zingine za karibu.Duru zasema kuwa mtu mmoja ameafariki kutokana na mkasa huo hata ingawa Radio Osotua haijaweza kudhibitisha hayo.

Kulingana na ripoti za awali mtu mmoja aliokolewa kwenye jengo hilo huku waokoaji wakiendelea kufukua vifusi vya jengo hilo.  Kuna hofu kuwa huenda kuna watu waliokwama ndani ya jengo hilo.Maafisa wa uokoaji kutoka kaunti ya Kiambu, msalaba mwekundu na idara ya polisi tayari wamefika kwenye eneo la  tukio.

Huo ni mkasa wa pili kutokea chini ya wiki moja baada ya jengo la ghorofa 7 kuanguka eneo la Seasons,Kasarani  siku ya Jumanne Novemba 14.Takriban watu 3 walikufa wakati jengo hilo lilipoporomoka. Watu wengine 6 waliokolewa kutoka kwa vifusi.

November 17, 2022