Kasarani Building Collapse

Waziri wa ardhi humu nchini Zacharia Njeru ameahidi kuwakabili wajenzi wote wanaoendeleza ujenzi ambao haujaafikia viwango hitajika.

Waziri njeru alisema haya baada ya kuzuru eneo la mkasa ambapo jengo la ghorofa saba liliporomoka katika eneo la Kasarani Jijini Nairobi.

Njeru aliyeandamana na gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, aidha amewataka wamiliki wote wa arthi wanaopania kutekeleza ujenzi, kufuata mawaidha ya wataalam na kuzingatia matakwa yaote ya ujenzi ili kuepuka Mikasa ya aina hii.

Kwa upande wake gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ameahidi kufunguliwa mashtaka kwa waliokuwa wakiongoza katika ujenzi wa jumba hilo, ambao waliendeleza kazi ya ujezi licha ya onyo na maagizo ya kusitisha ujezi huo kutolewa mara si moja na mamlaka ya ujenzi humu nchini NCA.

November 16, 2022