Rev, John Kiplimo

Jimbo Katoliki la Eldoret limepokea habari njema baada ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, kumteua Padre John Kiplimo Lelei kuwa Askofu Msaidizi. Kabla ya uteuzi huu, Padre Lelei alikuwa akihudumu kama Vicar Generali wa Jimbo hilo la Eldoret.

Taarifa rasmi kuhusu uteuzi huu zilitolewa na Vatican kupitia mtandao wa L’Osservatore Romano huko Rome saa nane kamili za saa za Afrika Mashariki. Mwakilishi wa Papa nchini Kenya na Sudan Kusini, Mwadhama Askofu Mkuu Bert van Megen, pia alitoa taarifa kuhusu uteuzi huu kwa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kenya (KCCB).

Majukumu ya Askofu Msaidizi, au kwa lugha ya kitaalam “Auxiliary Bishop”, ni kumsaidia Askofu wa Jimbo katika majukumu na shughuli mbalimbali za jimbo hilo. Uteuzi huu ni hatua muhimu katika kukuza na kuimarisha huduma za kiroho katika Jimbo la Eldoret.

Tunampongeza Padre John Kiplimo Lelei kwa uteuzi wake na tunamtakia heri katika majukumu yake mapya ya kiroho katika jimbo hilo.

March 27, 2024