Msajili mkuu mpya wa mahakama nchini Bi. Winfridah Mokaya

Msajili Mkuu mpya wa Idara ya Mahakama Winfridah Boyani Mokaya ameapishwa hii leo na kutwaa wadhifa wake rasmi katika hafla iliyoandaliwa kwenye majengo ya mahakama ya upeo jijini Nairobi mchana wa leo. Hafla ya kuapishwa kwake ilihudhuriwa na maafisa mbalimbali wa mahakama akiwemo jaji mkuu Martha Koome.

Bi. Mokaya ameahidi kuunga mkono uongozi wa idara ya mahakama na wafanyakazi wake ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Bi. Mokaya, ambaye amehudumu kama msajili wa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) na hakimu kwa zaidi ya muongo mmoja alisema uzoefu wake unampa fursa ya kutekeleza majukumu yake kwa uweledi.

Msajili mpya wa mahakama amechukua nafasi hii kutoka kwa Bi. Anne Amadi, ambaye alistaafu mwezi Januari 2024 baada ya kukamilisha muda wake wa kuhudumu wa mihula miwili.

March 25, 2024