Mfanyibiashara Jimmy Wanjigi amewaomba wanasiasa walioshindwa katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, kutotumia nyadhifa za utumishi wa umma kurejea uongozini na badala yake kuwaruhusu wakenya wengine waliohitimu kutwaa nyadhifa hizo.

Wanjigi ambaye alizungumza katika Kaunti ya Migori  siku ya Jumapili 10.Oktoba 2022, ameitaka tume ya utumishi wa umma PSC kuyatupilia mbali maombi ya walioshindwa katika uchaguzi na walio na nia ya kurejea katika nyadhifa za uongozi kwa kile alichokitaja kama njia za mlango wa Nyuma.

October 10, 2022