Huku Kenya ikiadhimisha siku ya utamaduni, baadhi ya wananchi wamechanganyikiwa kuhusu kinachosherehekewa hivi leo.Kuna wale ambao wanasema kuwa leo ni siku ya Huduma ila kuna wale ambao wanadai kuwa leo ni siku ya utamaduni.

Wakizungumza na waandishi wa habari,wananchi hao wamesema kuwa uwepo wa sikukuu nyingi humu nchini ndio unaleta mchanganyiko huo.Katika miaka za nyuma,siku hiyo ilikuwa ya kumsherehekea aliyekuwa rais wa pili wa taifa hili hayati Mzee Daniel Moi ila ikabadilishwa na kuitwa siku ya utamaduni ambapo jamii mbalimbali humu nchini zinapata fursa ya kusherehekea na kuonyesha tamaduni zao.

Kulingana na sura ya pili ya katiba kipengee cha tisa aya tatu siku za kitaifa ni tatu tu; siku ya madaraka ambayo huadhimishwa tarehe moja mwezi juni, siku ya mashujaa huadhimishwa okotoba, 20 na siku ya jamhuri huadhimishwa Desemba 12.

Aidha mnamo Desemba 19, 2019 ikulu iliarifu umma kuwa kikao cha mawaziri kilichoongozwa na rais Uhuru Kentyatta kiliidhinisha kubadilishwa kwa jina la sikukuu ya Moi ambayo iliadhimishwa oktoba 10 kila mwaka kuwa huduma day.Hii ilikuwa hatua ya kutekeleza pendekezo la hayati mzee Moi kuwa iwe siku ya kujitolea kutoa huduma bila malipo.

Wakati huohuo baraza hilo la mawaziri lilipendekeza Desemba 26 kuwa siku ya Utamaduni ila kwa sababu siku hiyo inaadhimishwa ulimwenguni kama siku ya boxing,Oktoba 10 ikaidhinishwa kuwa siku ya utamaduni huku siku ya Huduma ikiambulia patupu.

October 10, 2022