Waziri wa Hazina ya kitaifa John Mbadi amesimama kidete kuhusu matamshi ya hivi majuzi yenye utata yanayopendekeza kwamba serikali haiwezi tena kufadhili elimu ya bure ya shule za msingi na upili, akisisitiza kwamba ukomo wa bajeti ya Kenya unaifanya isiwezekane kufadhili elimu kwa kila mwanafunzi.

    Mbadi alifichua haya alipofika mbele ya kamati ya elimu katika Bunge la kitaifa siku ya Alhamisi na kusema kwamba mzigo wa kifedha wa elimu bila malipo ni mzito sana kwa Serikali kuudumisha, akidokeza kwamba hivi karibuni wazazi watalazimika kugharamika zaidi.

    Katika hotuba iliyolenga kufafanua msimamo wake wa awali, Mbadi alishikilia kuwa ingawa elimu inasalia kuwa kipaumbele kikuu cha serikali, nguvu ya sasa ya kifedha haiwezi kukidhi gharama kamili kwa kila mwanafunzi  ukweli ambao anawashutumu baadhi ya viongozi kwa kupuuza.

    July 26, 2025

    Leave a Comment