Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imetoa uchunguzi mpya ambao umeorodhesha maafisa wa polisi kama wataalamu wafisadi na wasio na maadili.

    Utafiti huo uliotolewa leo Jumanne umebaini kuwa ufisadi ni mojawapo ya visa vinavyoongoza katika sekta ya ajira nchini Kenya.

    Maafisa wa Mamlaka ya ukusanyaji Ushuru (KRA) walishika nafasi ya pili kwa 17.3%, Machifu waliibuka wa tatu kwa 16.2 huku maafisa wa ukaguzi wa kaunti (14.6%) na Wanasheria (14.1%).

    Vile vile, maafisa wa ukusanyaji ushuru wa kaunti, masoroveya, madaktari na wauguzi, wahasibu, wahandisi, walimu, wahadhiri na wanahabari pia waliorodheshwa miongoni kwa wataalamu wanaopokea rushwa na wasio na maadili mtawalia.

    EACC pia iligundua kuwa kuna uwezekano mkubwa wa hongo kutolewa katika afisi za utumishi wa umma, kwani Wakenya wanaombwa kutoa hongo ili kupata huduma za serikali.

    Kando na hayo, kupata nafasi katika Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kulionekana kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuombwa hongo.

    August 5, 2025